Kazi ipo! Taarifa ikufikie
kwamba kutoka kwenye bonge la pati la bethidei ya mtoto na mke wa
mwigizaji, William Mtitu, staa wa Bongo Dar es Salaam, Kulwa....
Kikumba
‘Dude’ amejikuta akimkatisha mauno mkewe, Eva hadharani kitendo
kilichozua minong’ono mingi baada ya mwanamama huyo kufanya kweli hadi
jamaa akamwambia yatosha.
Mke wa mwigizaji, William Mtitu, Yovitha akiwa na mwanaye Jane.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na wanahabari
wetu lilijiri nyumbani kwa Mtitu, Kigogo jijini Dar ambapo Dude alikuwa
Master of Ceremony ‘MC’ wakati mke wa Mtitu, Yovitha na mwanaye Jane
walizaliwa tarehe inayofanana ya Oktoba 31.
Mwigizaji wa Bongo Muvi, William Mtitu akiwa na mwanayeJane.
Katika sherehe hiyo iliyojaa kufuru ya
fedha na vituko vya mastaa, makundi mbalimbali yalipanda jukwaani na
kutoa burudani ya kufa mtu.Awali Dude alianza kwa kuitambulisha ngoma
yake mpya ya Kijijini kwa Bibi ambapo aliachia mistari mikali na
kuwapagawisha mashabiki wake kwa jinsi alivyokuwa ‘akirap’ kisha
kuiongoza vizuri shughuli hiyo.
Mshereshaji wa siku hiyo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ akimuomba mkewe, Eva akate mauno.
Ulipofika muda wa kukata mayenu ndipo Dude
akamwita Eva na kumwambia akate mauno mbele ya kadamnasi ambapo naye
alifanya kweli hadi akashangiliwa kabla ya Dude kumkataza kwa madai kuwa
ana shughuli nyingine nzito usiku huo.
Eva akikata mauno bila kupepesa macho.
Hata hivyo, Mtitu alionesha kutisha kwa
zawadi kubwa aliyomzawadia mwanaye baada ya kutakiwa kutangaza hadharani
ambapo aliinadi nyumba wanayoishi kuwa ndiyo zawadi pekee
aliyomwandalia mtoto wao kwani yeye na mkewe hawana muda mrefu duniani
huku akificha umri wa mkewe lakini mwanaye alikuwa anatimiza umri wa
mwaka mmoja.
Mshereheshaji ,'Dude' akionekana kama ni mwenye kuguna na kuchukua uamuzi wa kuzuia zoezi la mke (Eva) kukata mauno.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali huku washkaji zake
Mtitu wa Bongo Movie wakitoa hudhuru na kuwakilishwa na wachache kwa
sababu walikuwa safarini.
No comments:
Post a Comment