
Gari aina ya Toyota Hiace inayobeba abiria ikiwa imekandamizwa na container baada ya kuangukiwa
Kumetokea ajali mbaya jioni hii maeneo
ya Jeti Lumo mwisho wa lami Wilaya ya Temeke jijini Dar ambapo gari
kubwa la mizigo limeangukia Daladala iliyokuwa kituoni. Ajali
hiyo imetokea wakati gari hilo semi-trailer ikikata kona pale mwisho wa
lami ambapo kontena lilianguka na kutua juu ya bodi ya daladala.
Mtoa taarifa wetu amesema hali ni mbaya na bado haijajulikana idadi
ya vifo na majeruhi kwa ujumla. Pia gari imepondeka sana jambo ambalo
linaashiria hatari zaidi.
Kuna gari la kunyanyua makontena limeshafika pale lakini limeshindwa
kutoa msaada wa uhakika kutokana na kuzidiwa uzito na kontena ambapo
likijaribu kunyanyua kontena kushuka chini na kuzidi kuongeza maafa.
No comments:
Post a Comment