
Staa wa filamu Bongo,...
Blandina Changula 'Johari
STAA wa filamu Bongo,
Blandina Chagula ‘Johari’ amesema kwa sasa hataki kabisa kusikia habari
za mwigizaji, Chuchu Hans ambaye wamekuwa wakitifuana mara kwa mara
wakidaiwa kugombea penzi la Vincent Kigosi ‘Ray’.
Akikitemea cheche kinasa sauti cha paparazi
wetu baada ya kuulizwa kuhusiana na hatma ya malumbano yao ya mara kwa
mara na Chuchu, Johari alisema hataki kumzungumzia mwanadada huyo kwani
anampaisha bure.
Staa wa filamu Bongo, Chuchu Hans.
“Nimeamua nikae kimya kabisa wala sitaki kuzozana na mtu
nitajishushia hadhi kwa mashabiki wangu bure, siwezi kuwa namnufaisha
mtu kwa kumpandisha daraja kupitia mgongo wangu kutokana na malumbano,”
alisema Johari.
No comments:
Post a Comment