Maombi!
Staa wa sinema za Kibongo ambaye pia ni mwimba Injili, Sara Mvungi
anateseka hospitalini baada ya kusumbuliwa mara kwa mara na ugonjwa wa
nimonia (pneumonia) ambao umekuwa ukimkosesha amani na muda wa kufanya
kazi za kimaendeleo...
Staa wa sinema za Kibongo ambaye pia ni mwimba Injili, Sara Mvungi akiwa Hospitali ya TMJ.
Akizungumza kwa taabu na Ijumaa Wikienda akiwa amelazwa kwenye
Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar, Sara alisema kuwa ugonjwa
huo umekuwa ukimtesa hata kusipokuwa na baridi kutokana na hali ya hewa
ambayo haieleweki.
“Jamani kama ni kwa sababu ya baridi ndiyo
maana naumwa kiasi hiki hata siamini kwani hata kipindi cha joto,
najikuta naumwa ugonjwa huu,” alisema Sara akionekana kuwa na maumivu
makali.
Sara aliongeza kwamba, anamshukuru Mungu na ni mwema kuona sasa anaweza kupumua kwani hali yake ilikuwa mbaya kwa kuwa ugonjwa huo uliambatana na malaria kali.
Sara aliongeza kwamba, anamshukuru Mungu na ni mwema kuona sasa anaweza kupumua kwani hali yake ilikuwa mbaya kwa kuwa ugonjwa huo uliambatana na malaria kali.
Sara Mvungi akiuguza ugonjwa wa nimonia Hospitalini hapo.
Hata hivyo, Sara aliwashukuru wasanii waliokuwa wakifika hospitalini
hapo kumuona na Watanzania wote wanaomuombea na anawasihi wazidi
kumuombea. Sara amewahi kuripotiwa na gazeti hili kulazwa kwenye
hospitali hiyohiyo ya TMJ akisumbuliwa na ugonjwa huohuo hali
inayosababisha mashabiki wake kuhoji kwa nini ugonjwa huo umekuwa
ukimsumbua na wengine kumshauri kuhakikisha anautibu na kumaliza tatizo
hilo.
No comments:
Post a Comment