NI
Jumatatu nyingine tunapokutana katika uwanja wetu huu mzuri, tukijuzana
na kuelimishana kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo mapenzi. Mada yetu ya
leo ni kama inavyojieleza hapo juu....
Je, mara ya mwisho kwa wewe na mpenzi wako kutoka ‘out’ ilikuwa ni
lini? Una desturi ya kutoka na umpendaye, mkaenda mahali tulivu ambapo
mtapata muda wa kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu maisha na
mapenzi? Kama jibu lako ni hapana, unaishi kwenye mapenzi yaliyokosa
uhai. Maisha yanaenda kasi sana, wanandoa wengi au watu ambao wapo
kwenye uhusiano wa kimapenzi, wanajikuta wakikosa kabisa nafasi ya kuwa
pamoja kutokana na kila mmoja kuweka kipaumbele katika kazi, biashara au
shughuli nyingine za utafutaji pesa au malezi ya watoto.
Matokeo yake, watu wengi wanaishi kwa mazoea tu lakini katika uhalisia, mapenzi yanakuwa yamepungua sana au hayapo kabisa.
KUTOANA OUT HUFUFUA MAPENZI
Watafiti wa mapenzi wanaeleza kwamba
hakuna kazi ngumu kama kuishi pamoja wewe na mpenzi wako, iwe ni kwenye
ndoa au uhusiano wa kawaida wa kimapenzi kwani ni rahisi sana watu
kuchokana. Hata kama unampenda vipi, lazima kuna muda utamchoka au
utachoshwa na mazingira ambayo mmekuwa mkiishi siku zote.
Unapofikia hatua hii, kitu pekee kinachoweza ku-refresh akili na
hisia zako, ni wewe na umpendaye kutoka pamoja na kwenda sehemu tofauti
kama ufukweni, hotelini au sehemu yoyote tulivu ambayo mtakaa pamoja,
mtakunywa au kula na kufurahi. Kitendo hiki kinatajwa kuwa siri kuu ya
kufufua mapenzi na kuondoa ile hali
ya kuchokana.
Haijalishi umeishi kwa muda gani na mpenzi wako, hata kama mna miaka
kibao, lazima muendelee kutoana out mara kwa mara. Hata kama tayari
mmeshazaa watoto na wamekuwa wakubwa, suala la out halikwepeki kama
mnataka kuishi kwa amani na upendo. Wengi wanaamini kwamba mpenzi mpya
pekee ndiye anayetakiwa kutolewa ‘out’, jambo ambalo siyo sahihi.
Mkirudi, kila mmoja atashangaa kwamba mapenzi yake kwa mwenzake,
yatazidi maradufu, kama kulikuwa na migogoro ya hapa na pale, itaisha na
mtaendelea kuishi kwa amani na furaha.
SIYO LAZIMA UWE TAJIRI KUTOKA OUT
Wengi tunasumbuliwa na kasumba
kwamba ili kumtoa mpenzi wako out, ni lazima waleti yako iwe imejaa,
lazima mkatumie fedha nyingi au lazima umpeleke sehemu ya gharama. La
hasha, siyo lazima kabisa.
Kwa mfano, inakugharimu nini wewe na
mpenzi wako kutoka na kwenda ufukweni, mkaagiza soda, maji au vinywaji
mnavyovipenda, mkakaa kwenye mchanga wa bahari na kupunga upepo mwanana?
Hata kama hakuna ufukwe hapo mnapoishi, mnaweza kutoka na kwenda
sehemu yoyote tulivu, iwe ni kwenye uwanja wa mpira muda ambao hakuna
watu, sehemu za milimani au mahali popote ambapo mtakuwa wawili tu,
inatosha kabisa. Unaweza kununua matunda, vinywaji au vitafunwa
mnavyovipenda, mkaenda navyo mpaka sehemu mliyoichagua, siyo lazima uwe
na fedha nyingi.
MAMBO YA KUZINGATIA MKIWA OUT
Ili mtoko wako na umpendaye
ukamilike, kuchagua sehemu ya kwenda ni jambo la kwanza lakini kubwa
zaidi, lazima ujue kwamba mkiwa ‘out’, unapaswa kufanya nini ili mpenzi
wako afurahi na kufufua upya hisia za mapenzi ndani ya moyo wake.
Ukishindwa kujua nini cha kufanya na kipi hutakiwi kabisa kufanya
mkiwa out, badala ya kufufua mapenzi, unaweza kujikuta unaongeza ufa
hivyo ni lazima kila mmoja ajue anatakiwa kufanya nini anapokuwa out.
Tukutane wiki ijayo ili kujuzana nini unatakiwa kufanya na kipi
hutakiwi kabisa kufanya mnapotoka out na umpendaye. Vitabu vya ufundi
katika mapenzi vinapatikana kwa wakazi wa Dar. Piga namba za hapo juu
kwa maelezo.
No comments:
Post a Comment