
BAADA ya hivi karibuni
kumchana laivu Mkurugenzi wa Mwami Foundation, raia wa Kongo, Mwami
Rajabu, staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe anadaiwa
kumwangukia jamaa huyo na kumuomba msamaha
.
Staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe.
Kikizungumza na Risasi Mchanganyiko, chanzo makini kilidai kwamba
baada ya gazeti ndugu na hili kuripoti habari ya Wolper kumchana Mkongo
huyo huku akidai hana hadhi ya kuwa naye, wiki iliyopita alionekana
kwenye Hoteli ya Double Tree iliyopo Masaki jijini Dar ambako ndipo
alipofikia mwanaume huyo.
Kiliendelea kueleza kwamba mwanadada huyo alifika hotelini hapo kwa
ajili ya kumuomba msamaha Mkongo na alikuwa akifanya jitihada kubwa ili
asamehewe kwa kumtumia mwanamuziki wa FM Academia, raia wa Kongo, Patcho
Mwamba amuombee msamaha.
“Nimemuona Wolper akiwa na huyo Mkongo
kwenye hoteli hiyo aliyofikia ambapo kilichompeleka ni kuomba msamaha
kutokana na maneno aliyozungumza kwenye gazeti,” kilisema chanzo hicho.
Mwanamuziki wa FM Academia,raia wa Kongo, Patcho Mwamba.
Baada ya kupata habari hizo kutoka kwa chanzo, kwanza alitafutwa
Patcho Mwamba aliyedaiwa kusumbuliwa na Wolper akimtaka amuombee msamaha
kwa Mkongo huyo ambaye ndiye aliyemuunganisha naye ambapo alikuwa na
haya ya kusema:
“Siyo kweli kwamba Wolper anaomba msamaha mpaka sasa, kwani
ameshasamehewa na wako vizuri kabisa kwani siku ile gazeti lilipotoka tu
usiku wake tulikutana na Mkongo wakayamaliza.”
Kwa upande wa Mkongo alipoulizwa kuhusiana
na habari hiyo alisema ni kweli Wolper alikuwa hotelini hapo akiomba
msamaha huku akisema kwamba hakuwahi kuzungumza maneno kama hayo
yaliyoandikwa gazetini hivyo aliamua kumsamehe.
Mkurugenzi wa Mwami Foundation, raia wa Kongo, Mwami Rajabu.
“Nilimsamehe na sasa sisi ni marafiki wa kawaida tu siyo kimapenzi
kwa sababu mimi nina mke na watoto sita na ninamuogopa sana mke wangu
halafu hapa Tanzania sijaja kutafuta wanawake bali nimekuja kwa ajili ya
biashara lakini nawashangaa hawa wasanii wa kike kunipakazia kwamba
mimi nina uhusiano nao.
“Ipo siku nitafunguka mengi na watakoma kumendea waume wa watu,” alisema Mkongo.
Kujibu tuhuma hizo, Wolper alisema: “Watu wanasema sana lakini hakuna anayejua mimi na Mwami tukoje, kama ni bosi wangu au ni bwana wangu. Labda kama mtu aliniona nasalimiana naye akadhani nilikuwa naomba msamaha. Hakuna kitu kama hicho.”
Kujibu tuhuma hizo, Wolper alisema: “Watu wanasema sana lakini hakuna anayejua mimi na Mwami tukoje, kama ni bosi wangu au ni bwana wangu. Labda kama mtu aliniona nasalimiana naye akadhani nilikuwa naomba msamaha. Hakuna kitu kama hicho.”
No comments:
Post a Comment