
MSANII wa filamu Bongo, Halima Yahya ‘Davina’
amesema wanaomsimanga kuwa amepata mume kwa sababu yao hawana hoja kwa
sababu Bongo Movie Unity haina ubavu huo.
Msanii wa filamu Bongo, Halima Yahya ‘Davina’.
“Mimi sijatafutiwa mume na Bongo Movie, alinitafuta mwenyewe baada ya
kuniona kwenye muvi yangu ya Tone la Damu akiwa Italia, sasa nashangaa
na ninaumia ninaposikia eti Bongo Movie walinitafutia.
“Ukweli naombeni mniache kwa sababu hakuna aliyehusika kwa kitu
chochote kunikutanisha na mume wangu, hivyo acheni kunisengenya na mimi
siringi kwa chochote kama ni kutoka huko kwenye kundi ni maamuzi yangu
maana sikuwa naona faida yoyote,” alisema Davina.
No comments:
Post a Comment