
WAKATI nyota wa muziki wa
Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ akikamatwa Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa na madawa ya kulevya akiwa njiani
kuelekea Mbeya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ aliyekuwa amemfungulia kesi ya
kumpiga katika kituo cha Polisi cha Oysterbay, amefuta shauri hilo na
kumsamehe.
Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Akipiga stori na gazeti hili, Ray C alisema ameamua kumsamehe kwa
sababu yeye ni mtu wa Mungu na anaamini yanayomtokea ni ishara ya
kumtambulisha kuwa matumizi ya dawa za kulevya hayafai.
“Mimi ni mtu wa Mungu, nimemsamehe na wala sitaki kesi naye, lakini
kumsamehe mimi peke yangu hakusaidii, Watanzania wote kwa pamoja
tumuombee ili jambo hili limalizike na likiisha, ninamuomba aje
tushiriki pamoja katika tiba ya Methadone,” alisema.
Ray C maarufu kama kiuno bila mfupa, alitoa
kauli hiyo muda mfupi baada ya kuandika waraka katika akaunti yake
kwenye mtandao wa Instagram, akimsihi Chid Benz kuachana na matumizi
hayo ya madawa ya kulevya.
Nyota wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’.
“Pole kaka yangu Chid Benz, naumia kuona tatizo ulilokuwa nalo bado
haujalitafutia jibu, mimi ni dada yako na tumeshafanya kazi pamoja.
Tatizo ulilonalo na mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu
nilijitambua na kutafuta suluhu, nimejaribu kila njia kukushauri badala
yake ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani kwangu,”
yalisomeka baadhi ya maandishi yake mtandaoni.
Ray C aliendelea kuandika kuwa kitendo
cha kukamatwa kwake na madawa hayo kitakuwa ni jibu zuri kwake kuwa
anakoenda si salama na kumtaka abadili njia na kuungana naye kwenye tiba
ya Methadone kwani ndiyo kiboko ya madawa ya kulevya.

Kamanda Nzowa.
Chid Benz alikamatwa akiwa na kete 14 za madawa ya kulevya pamoja na
misokoto miwili ya bangi hadi gazeti hili linakwenda mtamboni, alikuwa
bado hajafikishwa mahakamani kukabiliana na tuhuma hizo.
No comments:
Post a Comment