STAA wa sinema za Kibongo, Aisha Bui amefunguka kuwa
hivi karibuni aliangusha timbwili la kufa mtu kudai fedha zake za
filamu aliyocheza kwa sababu fedha aliyotumia kuandaa filamu hiyo
hakuhongwa na mwanaume....
Staa wa sinema za Kibongo, Aisha Bui akiwa katika ofisi za kusambazia filamu za Yuneda, Mbagala jijini Dar.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Aisha ambaye alianzisha timbwili
katika ofisi za kusambazia filamu za Yuneda, Mbagala jijini Dar, alisema
kuwa aliumia kuona anazungushwa kuhusu malipo wakati yeye hutafuta
chapaa kwa jasho lake mwenyewe tofauti na wasanii wengine ambao fedha
zao ni za kupewa na wadau.
Staa wa sinema za Kibongo, Aisha Bui akionekana kuwa ni mwenye gadhabu
“Unajua naumia sana hela yangu siyo kwamba nilihongwa na wanaume bali
nilitafuta kwa jasho langu hivyo mtu anapokuwa na lengo la kunidhulumu
naumia mno na ninashikwa na hasira sana,” alisema Aisha Bui.
No comments:
Post a Comment