Bomu lililotengenezwa kienyeji kama linavoonekana katika picha.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akipata maelekezo kutoka kwa
mtaaram wa mabomu ambaye ni kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania(JWTZ) kabla ya kulitegua bomu hili.
Hili
ni eneo la tukio ambalo limezungushiwa mkanda huu wa polisi uliandikwa
hairuhusiwi kupita eneo hili,Lakini chini ya huo mti kama inavoonekana
katika picha kukiwa na udongo umetifuliwa ndipo mahara ambapo lilitegwa
bomu hili la kutengenezwa kienyeji pia hapo ndipo huwa wanakaa askari wa
Usalama barabarani kwa kujikinga na jua ama kupumzika pindi wanapokuwa
kazini
Bomu lililotengenezwa kienyeji
Mtaaramu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiweka vifaa vyake vya kutegulia bomu hilo lililo tengenezwa kienyeji.
Mtaaramu
toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiwa anaonyesha umahili
wake alionao aweze kulitegua bila kuleta madhara yoyote yale katika
jamii
Jeshi la polisi kwa kushirikiana na Jeshi
la Ulinzi la wananchi Tanzania(JWTZ) wamefanikiwa kulipua bomu
lililotegwa katika eneo la kituo cha kurushia matangazo kilichopo
mshangano cha shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Songea Mkoani Ruvuma
siku ya jana majira ya saa moja jioni.
Bomu hili linalosadikiwa kutengenezwa
kienyeji nawatu wasiojulikana lilitegwa hatua zinazokadiliwa thelathini
kutoka kitika kituo kilipo katika eneo ambalo askari wa usalama
barabarani wanakaa kwa ajili kufanya kazi zao za kila siku.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo
Msikhela amesema kwamujibu wa wataalamu wa milipuko kutoka jeshi la
Ulinmzi la wananchi wa Tanzania bomu hili linaonekakana limetengenezwa
kienyeji.
ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa jeshi la polisi ili liweze kuwabaini watu waliowalipua kwa bomu lililotengenezwa kienyeji askari polisi watatu wakiwa katika doria katika kata ya misufini manispaa ya songea.
ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa jeshi la polisi ili liweze kuwabaini watu waliowalipua kwa bomu lililotengenezwa kienyeji askari polisi watatu wakiwa katika doria katika kata ya misufini manispaa ya songea.
Msikhela amesema Jeshi la polisi linafanya
jitihada za kuwapata watu hawa wanaohusika na mtandao huu wa utegaji wa
mabomu na ulipuaji, Aidha ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa Jeshi la
Polisi ili liweze kuwabaini watu wanaousika na matukio ya namana hii.
Na hii ni mara ya pili katika manispaa ya
songea kutokea kwa matukio haya ambapo tarehe Oktoba 16 mwaka huu askari
watatu wa jeshi la polisi katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,
walijeruhiwa kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono
ambalo lilisadikiwa kutengenezwa kienyeji, katika eneo la matarawe mjini
songea mkoani Ruvuma.
Askari hao walikutwa na mkasa huo saa moja
na nusu usiku wakati wakiwa katika doria ambao ni WP Felista Abel, PC
John Kaduma na PC Ramadhani Ally
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea
Joseph Mkirikiti akizungumza na mtandao huu wa demasho kwa njia ya simu
amesikitishwa na kitendo hicho cha utegeji wa Mabomu ikiwa nikutaka
kuhatarisha amani iliyopo katika mkoa huu wa Ruvuma.
Aidha amesema serikali kupitia vyombo vyake
vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata walewote
wanaohusika na vitendo hivi.
No comments:
Post a Comment