WATU 10 wamepoteza maisha huku zaidi ya 300 wakiwa hawajulikani
walipo baada ya kutokea maporomoko ya udongo katikati mwa nchi ya Sri
Lanka leo.Maporomoko hayo yametokea kufuatia kunyesha kwa mvua kubwa ambapo
takribani nyumba 140 zimefunikwa na udongo katika Wilaya ya Badulla.
Msemaji wa Kitengo cha Kukabiliana na Maafa nchini humo, Sarath Kumara amethibitisha taarifa hizo.
Vyombo mbalimbali vya uokoaji vipo eneo la tukio kujaribu kuokoa majeruhi wa tukio hilo.
Maporomoko hayo pia yamelikumba shamba kubwa la chai la Meeriyabedda
lililopo karibu na mji wa Haldummulla, uliopo kilomita 200 (maili 120)
mashariki mwa mji mkuu Colombo.
No comments:
Post a Comment