NAAM!
kama kawaida tumekutana tena kwenye kona yetu ili tujuzane machache,
tumeona wenyewe jinsi sikukuu ya Xmas ilivyokwisha, je mwenzangu
ulipata au ulipatikana. Nasikia wapo waliopombeka mpaka wakazimika, mmmh
makubwa watu wengine hawanywi mpaka sikukuu....
Hivyo unakunywa mpaka unazimika unategemea nini, wenzako wakubebe eeh
uwape shida kwa raha zako za kijinga, haipendezi jamani kunyweni kadri
ya uwezo wenu siyo lazima kikiwa kingi basi lazima ukimalize. Kunywa na
kula kwa uwezo wako.
Si unakumbuka nilikueleza nilivyomuokoa mwanamke mlafi kila kitu
kwake “hamu” yaani lazima kiingie mdomoni. Sasa nisingetokea kama siyo
siku ya pili kwenda kupigwa bomba ni nini, tuacheni tamaa kwa kutaka
kumkomoa mtu bila kujua mfukoni kwake yupo vipi.
Matokeo yake ndiyo hayo unajidhalilisha unakunywa mpaka unazimika, ya
X-mas yamepita, sasa tuulizane sisi wenyewe katika pitapita yetu ya
kuchuna mabuzi, tumepata nini, je mwaka huu ulikuwa wa faida au hasara
kila siku kukopwa hata pesa ya sabuni ya kufulia nguo ya ndani huna.
Usikubali kufanya kazi kwa kujifanya ubao wa matangazo kila mwenye
macho ajisomee utazeeka na ubakie shangingi mstaafu mwenye sifa ya
kukopwa na kupigwa mtungo tu, huna lolote la maana!
Lazima sasa hivi tujiulize tumekwama wapi na kipi ulichokifanya kukuingizia kipato, usiwe wa kwenda kila siku hujui mwisho wa mwaka kazi yako imeingiza au imetoa.
Lazima sasa hivi tujiulize tumekwama wapi na kipi ulichokifanya kukuingizia kipato, usiwe wa kwenda kila siku hujui mwisho wa mwaka kazi yako imeingiza au imetoa.
Kama haina faida badili kazi nyingine siyo lazima upigwe na baridi na
kugeuzwa shamba la mbu bila faida. Usiogope kujaribu biashara nyingine
huenda ikakutoa na hiyo igeuke starehe badala ya kazi.
Narudi kwako wewe wa ndani, umeumizwa mara ngapi katika ndoa yako,
umegundua kosa lako nini lililomfanya mumeo asirudi mapema au kulala
nje, au kazi yako kulia tu hujui lolote, haipendezi lazima ujiulize
iweje zamani alikuwa mapenzi motomoto leo hii yamepungua na kuwa penzi
la mgao kama umeme.
Kama utakuwa kimya kutegemea Mungu yupo nawe hujui matatizo yako talaka hiyoo unaiita mwenyewe.
Mwaka umekwisha, umegundua udhaifu wako. Hebu muda huu mchache utumie kujiuliza hata kukaa na mwenzako na kumuuliza mpenzi hebu nieleze kosa langu.
Mwaka umekwisha, umegundua udhaifu wako. Hebu muda huu mchache utumie kujiuliza hata kukaa na mwenzako na kumuuliza mpenzi hebu nieleze kosa langu.
Kwa vile ni mwisho wa mwaka kila mtu atatumia nafasi hii kuzika tofauti zake na kuingia mwaka na furaha na amani ya moyo.
Nawe uliyefanikiwa utumie mwaka huu kwa mafanikio zaidi na kurudi
ulikotoka, siku zote kufika kileleni ni rahisi lakini kukaa kileleni ni
kazi, ni wakati wa kuimarisha yote uliyoyafanya mpaka ukajengewa nyumba
au kununuliwa gari usibweteke gari zuri likaozea uani.
Yangu ni hayo kwa mwaka 2014 na kuwashukuru wote waliofuata, wengi
wamefanikiwa na waliopuuza sasa wanajuta. Si mwingine ni mimi anti Nasra
Shangingi mstaafu. Heri ya mwaka mpya.
No comments:
Post a Comment