
Baada ya wiki iliyopita kuwaletea wasanii 7 matajiri Afrika. Wiki hii tunawaletea marais 6 wa kwanza wanawake katika nchi zao.......
Sheik Hasina Wajed.
Sheik Hasina Wajed ANA miaka 67. Kabla ya kuwa rais wa sasa wa
Bangladesh kwa uchaguzi wa mwaka 2009, aliwahi kuwa waziri mkuu mwaka
1996 akaondolewa madarakani kutokana na nchi kukithiri rushwa. Mji Mkuu
wa Bangladesh ni Dhaka.
Tarja Kaarina Halonen.
Tarja Kaarina Halonen NI rais wa nchi ya Finland ambayo mji mkuu wake
ni Helsinki. Ana miaka 71. Amekuwa rais wa nchi hiyo tangu mwaka 2000
akiuweka vizuri uchumi wake.
Cristina Fernández de Kirchner.
Cristina Fernández de Kirchner Alizaliwa Februari 19, 1953. Ni rais
wa kwanza mwanamke nchini Argentina yenye mji mkuu unaoitwa Buenos
Aires. Aliingia madarakani mwaka 2009.
Dilma Vana Rousseff.
Dilma Vana Rousseff Ni rais wa Brazil aliyeibuka na ushindi wa
asilimia 53 katika matokeo ya uchaguzi Jumapili iliyopita. Ana miaka 67.
Ni mwanamke wa kwanza kuwa rais nchini mwake. Mji mkuu wa Brazil ni
Brasilia.
Ellen Johnson Sirleaf
Ellen Johnson Sirleaf NI rais wa Liberia, nchi iliyopo barani
Afrika.Mji mkuu ni Monrovia. Alizaliwa Oktoba 29, 1938. Ni rais wa
kwanza mwanamke Afrika. Aliwahi kuwa waziri wakati wa utawala wa William
Tolbert.
Park Geum-hye.
Park Geum-hye NI rais wa Korea Kusini, mji mkuu ni Seoul. Ana miaka
62. Aliingia madarakani mwaka jana kwa ushindi wa asilimia 50.6. Nchi
yake ikidaiwa kuwa na nguvu kubwa ya kiuchumi na kijeshi, hasa kwenye
silaha za nyuklia.
No comments:
Post a Comment