Mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na shostito wake, Aunt Ezekiel wakiangusha kicheko katika kaburi la marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’.
Ni vigumu kutokea lakini imetokea! Wakati dunia ikisherehekea ujio wa mwaka mpya wa
2015....
mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na shostito wake, Aunt Ezekiel
walionesha jambo tofauti kufuatia kutinga kwenye kaburi la aliyekuwa
nyota wa Bongo Fleva, marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’ na kutumia muda
mwingi kucheka na kutuma meseji kwa simu wakiwa juu ya kaburi hilo.
ENEO LA TUKIO
Tukio hilo lililonaswa zimazima, lilijiri Januari Mosi, mwaka huu kwenye
kaburi la Ngwea lililopo katika Makaburi ya Kihonda mjini Morogoro.
ILIVYOKUWA
Aunt ndiye aliyeanza kutia timu
kwenye makaburi hayo na kukaa. Baadhi ya ‘kruu’ ya Wema, akiwemo Petit
Man nayo ilifika na kuungana na Aunt.Baada ya dakika tatu, Mama la Mama,
Wema aliwasili akiwa ndani ya nguo isiyokuwa ya mtoko, akakaa upande wa
pili wa kaburi. Yeye na Aunt walikaa kwa kupeana ubavu.
CHA AJABU SASA
Awali ilidaiwa kuwa, kruu hiyo
ilipanga kuwa baada ya kufika kwenye kaburi hilo wangefanya dua fupi kwa
ajili ya kumwombea marehemu apumzike kwa amani huko aliko.Lakini cha
ajabu, kabla ya ibada hiyo, Wema, Aunt na wafuasi wao walikuwa wakipiga
stori za hapa na pale na katika hali ya kushangaza zaidi, ilifika mahali
wakaanza kucheka kile kicheko cha kuvunjika mbavu bila shuhuda wa tukio
hili kujua nini hasa kilichokuwa kikiwachekesha!
Wakizidi kucheka katika kaburi hilo.
Baadhi ya wapita njia waliokuwa wakikatiza karibu na makaburi hayo,
nao walipigwa na butwaa kuwaona watu hao, walioamini ni ndugu wa
marehemu, wakiangua vicheko kama hawana akili nzuri. kwa nukta kadhaa
walisimama na kushangaa kabla ya kuendelea na ‘hamsini zao’.-
WEMA ATUMIA SIMU KUFICHA USO
Ni dhahiri kuwa,
Wema alijishtukia kuwa kitendo cha kucheka juu ya kaburi hakikuwa na
ujazo wa kiungwana hivyo haraka sana aliweka simu sehemu ya midomoni na
kumfanya asionekane kwenye kamera kwamba alikuwa akicheka. Miwani ya jua
aliyovaa pia ilimsaidia.
Wakati Wema akionesha ubinadamu huo, ‘mwenzangu na mimi’, Aunt yeye
alijimalizia kiu yake ya kicheko mpaka pale alipoamua mwenyewe kuacha na
si kwa kuogopa kamera wala malaika waliolizunguka kaburi lile (kama
wapo) la mmoja wa marapa bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania.
WEMA AJIELEZA
Baada ya wote kuacha
kucheka na kila mmoja kuchukua nafasi ya ubinadamu, mwandishi wetu
alimuuliza Wema ni kwa nini walionesha kuwa na furaha juu ya kaburi la
staa huyo.Wema: “Tumepita hapa ili kumuombea ndugu na rafiki yetu
Mangweha hivyo hatuna lengo lingine zaidi ya hilo.“Ishu ya kupiga stori
na kucheka, tusingeweza kuacha kuongea eti kisa tupo kaburini, maana
kila kitu lazima kijadiliwe hata kukaa hapa tumekaa kwa sababu
tunafarijika kuona kaburi la mwenzetu.”
Albert Mangweha ‘Ngwea’ enzi za uhai wake.
KWA NINI WALIFANYA ZIARA KABURINI KWA NGWEA?
Awali, mastaa hao na wapambe wao walikuwa na shoo ya kuukaribisha Mwaka
Mpya iliyofanyika Desemba 31, 2014 ndani ya Ukumbi wa Matei Lounge
mjini Dodoma.Wakiwa wanarudi Dar, walipiga kituo mjini Morogoro ambapo
miongoni mwa mambo waliyokuwa nayo kwenye ratiba ni kulitembelea kaburi
la Ngwea na kuangusha dua fupi.
Hata hivyo, baada ya yote hayo, kundi hilo la Wema na watu wake
hatimaye walifanya dua fupi ya kumuombea malazi mema Albert Mangweha.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Mangweha alikuwa msanii wa
Bongo Fleva. Akiwa na miaka 31 alifariki dunia, Mei 28, 2013 nchini
Afrika Kusini. Chanzo cha kifo chake inadaiwa ni matumizi
yaliyopitiliza ya madawa ya kulevya. Alizikwa Morogoro, Tanzania, Juni
6, 2013.
No comments:
Post a Comment