Jeshi la polisi kushirikiana na waandishi wa habari kilifanikiwa kunasa tukio la aina yake baada ya kijana
mmoja aliyefahamika kwa jina la Joni Simon kunaswa na kitita cha fedha
bandia akitaka kuwekewa katika simu yake ya mkononi kupitia mtandao wa
Tigo Pesa, tukio lililotokea Sinza Afrika Sana jijini Dar..
Mashuhuda waliwatonya waandishi wa habari kuwa kijana huyo alinaswa katika duka moja la
Tigo Pesa lililopo maeneo ya Kona Bar karibu na Hoteli ya kisasa ya
Atriums.Baada ya kuwekewa pesa katika simu yake, alitoa ‘mkwanja huo
bandia’ na kumkabidhi jamaa wa Tigo Pesa, lakini alizitilia mashaka
fedha hizo na kulazimika kumzuia asiondoke kwanza, lakini jamaa huyo
akataka kutimua mbio.
Kabla hajafanya hivyo, jamaa wa Tigo Pesa alimrukia na kumshika huku
akipiga kelele za kuomba msaada ndipo akaupata kutoka kwa wauza chips
walio karibu.Ndipo simu ilipopigwa kwa polisi wa kituo cha Mabatini
Kijitonyama ambao wakiongozwa na Kamanda Rashidi wakaingia eneo la tukio
mara moja lakini walilazimika kutumia bunduki kumtisha ili kumtuliza
kijana huyo na kumtia mbaroni.
Baada ya kumpekua walimkuta na kiasi cha zaidi ya shilingi laki
mbili, zote zikiwa bandia na waliondoka naye kuelekea kituoni kwa
mahojiano zaidi kabla ya hatua nyingine za kisheria kufuata.
RPC Wambura.
Tukio hilo limetokea siku chache tu baada ya mtu mmoja huko mkoani
Mwanza, kukamatwa akiwa na kiasi cha shilingi milioni 400 za Kitanzania,
ambazo pia ni bandia, zilizokusudiwa kuingizwa katika mzunguko wa
fedha.
No comments:
Post a Comment