Mkurugenzi wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’ Asha Baraka.
MKURUGENZI
wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’ na...
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba
wamewatolea uvivu mastaa wanaojihusisha na utumiaji wa madawa ya
kulevya (mateja) na kuwataka waache wenyewe.
Wakizungumza katika mahojiano maalum na mwanahabari wetu kwa nyakati
tofauti, Januari 5, mwaka huu, wakurugenzi hao walikiri kuwa tatizo la
mastaa wanaobwia unga ni kubwa na halitapungua kama juhudi za makusudi hazitafanyika.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
Kwa upande wake Ruge, alisema asilimia kubwa ya watu ambao wanatumia
madawa ya kulevya walianza kwa kuvuta bangi na baada ya kuizoea ndipo
wakaanza kuchanganya unga kwenye msokoto na baadaye kujikuta wanajidunga
madawa ya kulevya.
“Kuna wasanii wengi sana wanaotumia unga ukiachilia mbali hao kina
Ray C, Chid Benz, Diouf na Aisha Madinda (marehemu) ambao waliwahi
kuripotiwa, tunawajua ingawa hawataki kujianika, wabadilike,” alisema
Ruge.
Asha yeye alisisitiza suala hilo kwa kutoa mifano hai. Alisema kabla
Aisha Madinda hajafariki, alifanya kila juhudi za kumnusuru na utumiaji
wa madawa lakini kuna watu walikuwa wakimpiga vita na kujikuta
wakimtorosha.
“Huwezi amini jinsi ninavyopigania vijana wangu kutoka kwenye wimbi
hilo maana nilishawahi kumchukua Banza na Msafiri Diouf enzi hizo
Muhimbili (Hospitali ya Taifa) walikuwa hata hawajaanzisha kitengo cha
kuwapatia dawa za kuondoa sumu hiyo.
No comments:
Post a Comment