
UNENE wa kupindukia ni ugonjwa na wasomaji wengi wametaka tuwasaidie kuwaeleza njia za kupunguza au kuondoa tatizo hilo.Kuna njia nyingi sana ambazo hutumiwa na watu ili kupunguza mwili na tumbo....
Zipo njia za kutumia madawa au kahawa, chai ya kupunguza uzito na
vinginevyo ambazo huwa si za kudumu na hata baadhi huwa na
madhara.Lakini njia hii ifuatayo unaweza kuifanya ikawa ni maisha yako
ya kila siku ikazoeleka na ukawa unaishi hivyohivyo bila kuongezeka
uzito wa mwili.
Tutatoa mfano wa kupunguza uzito kwa muda wa siku 7. Mambo muhimu ya
kuzingatia ni kwamba, kupungua uzito kunategemea kiwango cha mafuta
mwilini (body fat), uzito wa mtu, kalori anazohitaji kwa siku, BMI yake
pamoja na lengo la mtu kutaka kupunguza uzito.
Nahitaji kupunguza kiwango cha mafuta mwilini kwa kiasi gani? Kwa
mfano wengine wanahitaji kupunguza asilimia 10, 20 au 25 ya kiwango cha
mafuta mwilini. Kwa maana hiyo, si kila mpangilio wa ulaji (diet plan)
humfaa kila mtu, inaweza ikawafaa baadhi na isiwafae wengine.
Jambo lingine la kuzingatia ili kupungua uzito ni kufuata ushauri wa
wataalamu wa lishe, madaktari, wataalamu wa mazoezi na kadhalika.
Ufuatao ni mfano wa njia ya kupunguza unene au diet plan. Kila siku
unahitaji kunywa kikombe kimoja cha kahawa na ni vizuri kubadilisha
unywaji wa kahawa kwa chai, yaani kama leo utakunywa kahawa kesho kunywa
chai na kadhalika.
Kwa wale wenye ugonjwa wa shinikizo la damu, ugonjwa wa wasiwasi na
kadhalika, wanashauriwa kuepuka kahawa kabisa na hivyo wanywe chai.
Wagonjwa wa kisukari wanaweza kunywa chai au kahawa kwa kukamulia ndimu
au limao ndani yake na hivyo kuongeza ladha.
Siku ya kwanza:
Siku ya kwanza:
Mazoezi: Wale wenye matatizo ya kiafya ya mapigo ya moyo au wale
ambao walishawahi kuugua hapo awali matatizo ya moyo na wagonjwa wa
pumu, ni vyema wafanye mazoezi chini ya uangalizi wa wataalamu wa
mazoezi pamoja na kushauriana na daktari.
Tembea kwa muda wa dakika 30 asubuhi au jioni kabla ya kula chakula
chochote. Kwa wale wenye mashine ya kutembelea ya tredmill wanaweza
kutembea kwa muda wa dakika 30 kwa kuanza na kasi ndogo. Unaweza pia
kukimbia kwa muda wa nusu saa au kukimbia kwenye mashine ya tredmill kwa
muda wa nusu saa.
No comments:
Post a Comment