Kocha mpya wa Simba, Goran Kopunovic.
KOCHA mpya wa
Simba, Goran...
Kopunovic anaratajia kutua nchini leo saa 1:30 asubuhi
akitokea nchini Hungary tayari kuingia mkataba na klabu hiyo na moja kwa
moja kwenda Zanzibar.Kopunovic anatua nchini akiwa na ‘hasira’ au
‘kisasi’ kwa watani wa jadi wa Simba, Yanga kwa kuwa waliwahi ‘kumtema’.
Miaka mitatu iliyopita, Yanga ilifanya mazungumzo na Kopunovic raia
wa Serbia ili atue nchini kuinoa. Lakini wakati akiajiandaa kuja nchini,
ikaachana naye na kumchukua Ernie Brandts ambaye alikuwa mpinzani wake
mkubwa.
Wakati huo Brandts raia wa Uholanzi alikuwa akiinoa APR ya Rwanda
iliyobeba ubingwa na Kopunovic akiwa na Polisi Rwanda iliyoshika nafasi
ya pili.Chanzo kimeeleza, Kopunovic amekubali kuja nchini, atawasili kwa
‘mwewe’ wa Qatar Airways lakini amesisitiza, anakumbuka Yanga
walivyowahi kumfanyia.
“Amesema anaijua Simba, hata wakati fulani alikuwa anakuja
kuifundisha Yanga, halafu wakamuacha mwishoni. Ila amesisitiza anapenda
soka la Tanzania,” kilieleza chanzo ndani ya Simba.
Kocha aliwahi kucheza na Yanga mechi ya kirafiki akiwa Polisi Rwanda
na kupoteza kwa mabao mawili. Anatarajia kusaini mkataba leo au kesho
kulingana na makubaliano yake na uongozi wa Msimbazi.Halafu atakwenda
kuungana na kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka leo kwenda Zanzibar
kwa ajili ya michuano ya Mapinduzi.
No comments:
Post a Comment