

Ndugu na jamaa wa watu
waliokuwa kwenye Ndege ya....
AirAsia wakiwa na simanzi baada ya kupata
taarifa za kupatikana kwa miili baharini.
JITIHADA za kuopoa miili kutoka katika Ndege ya AirAsia QZ8501
iliyoanguka baharini Jumapili iliyopita ikiwa na watu 162 zimeendelea
kukwamishwa na hali mbaya ya hewa.
Ndege hiyo ilianguka katika Bahari ya Java nchini Indonesia na hali
ya dhoruba katika eneo la uokoaji imezida kukwamisha zoezi hilo.
Mwili wa mmoja wa watu waliokuwa kwenye ndege ya AirAsia ukielea katika Bahari ya Java.
Mamlaka nchini Indonesia yamethibisha kuwa mabaki yaliyoonekana majini eneo la Borneo ni ya ndege iliyopotea ya AirAsia.
Rais wa Indonesia, Joko Widodo, ameahidi kuendelea kufanya uchunguzi
wa kina kwa kutumia meli na helkopta kuhakikisha miili ya watu waliokuwa
kwenye ndege hiyo inapatikana.
Maombolezo ya pamoja yanatarajiwa kufanyika leo huko Surabaya nchini
Indonesia na Gavana wa Jimbo la Java Mashariki, Soekarwo ameeleza kuwa
sherehe zote za Mwaka Mpya zimesitishwa kutokana na ajali hiyo ya
AirAsia.
No comments:
Post a Comment