
MARA kadhaa utakuwa umekutana na marafiki wanaozungumza maneno mengi kuhusu ngono. Baadhi wanapozungumza, wanaonyesha wazi kutopendezwa na hali yao ya kupenda ngono kupita kiasi, lakini wengine huongea kwa kujisifu kwa vile ni mahodari wa kushiriki tendo lile...
Wanaojisifu, ndiyo hawa huja na kauli kuwa wao hobi yao ni mapenzi.
Neno hili, hobi, ni la kiingereza linalomaanisha kitu ambacho mtu
anakipenda. Mtu atasema hobi yake ni kusoma, mwingine michezo au muziki
na kadhalika. Kila mmoja anacho akipendacho, yaani akikipata hicho, roho
yake inakuwa raha burudani.
Katika siku za hivi karibuni nimeshuhudia mastaa wawili wakizungumzia
ngono, ambao ni Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Baby Madaha. Lulu alisema
ngono zimekuwa zikimtesa kiasi kwamba kila mara hujikuta katika hali ya
kutaka kufanya mapenzi, kitu ambacho mwenyewe anaamini ana jini mahaba.
Kwa upande wake, Baby Madaha yeye anakuja live kabisa akidai kwamba,
kwake yeye, kufanya mapenzi ni hobi yake, yaani ndicho kitu
anachokipenda kuliko vitu vingine vyote duniani, yaani kwake yeye,
kushiriki tendo akiwa na mwenzi wake ndo faraja yake.
Wazungu
wana msemo wao mmoja maarufu unaosema too much of anything is harmful,
kwa tafsiri isiyo rasmi ni kwamba kitu chochote ukikizidisha,
kitakupatia madhara.
Kushiriki tendo la ndoa ni kitu kinachofurahiwa na wengi, wake kwa
waume, ingawa kila mmoja ana aina ya ufurahiaji wake. Wapo wanaozidisha
ufanyaji wa tendo hili kutokana na sababu mbalimbali. Kuna wanaofanya
hivi ili kujipatia kipato. Anakesha usiku kucha akibadilisha wanaume kwa
ajili ya kipato.
Lakini wapo ambao wanapenda kushiriki tendo kwa sababu ya raha tu na
siyo kingine. Kwa wote wenye aina hii ya mahitaji, wanaambiwa kuwa wana
pepo la ngono!Sisemi kuhusu machangudoa, kwa sababu wote tunajua kuwa
hawa wanafanya hivi ili kupata hela, nazungumza na wanawake na wanaume
ambao muda wote wanawaza ngono na hata wakifanya hawaridhiki. Anatoka
kuchepuka sehemu, lakini anapopanda kwenye daladala macho yake
yanavutiwa na mwanamke mwingine na yupo tayari kumtongoza na kulazimisha
kwenda naye muda uleule.
Ukimuona mtu wa aina hii, ni wa kumsaidia kwa sababu huo ni ugonjwa.
Binadamu anao uwezo mkubwa wa kuhimili hisia za mapenzi yake. Wale
waliooa au kuolewa wanaweza kuwa mashahidi wazuri wa hili. Unaweza
kukuta wanandoa wanakaa hata wiki mbili bila kukutana, ingawa wanalala
kitanda kimoja.
Tendo la ndoa ni kitu cha afya. Mwili hujiweka vizuri zaidi kwa
ushiriki wake, lakini unapozidisha dozi, ni tatizo. Ugonjwa huu
unatibika, nenda hospitali, onana na daktari bingwa wa saikolojia,
atakueleza kwa nini unakuwa hivyo ulivyo na nini suluhisho la kudumu.
No comments:
Post a Comment