Kocha Patrick Phiri.
KOCHA Patrick
Phiri amesema amesikitishwa na taarifa za...
kuachishwa kazi Simba, lakini
angependa kumalizana vizuri na uongozi wa klabu hiyo.Phiri raia wa
Zambia amesema tayari amepewa taarifa hizo na mmoja wa viongozi wa
Simba, lakini si taarifa rasmi ya barua.
“Nimeelezwa, si kitu cha furaha. Nasikia majonzi kwa kuwa niliona
ninaweza kubadilisha mambo baada ya kupata kikosi kipya.“Nilikuta kikosi
kipya, tukawa tunaanza kuzoeana lakini tukafanya tena mabadiliko, hivyo
ndiyo tulikuwa tumeanza kutengeneza timu tena, tukafungwa na Kagera.
“Sidhani kama tumefanya vibaya sana, lakini siwezi kuzuia uongozi
unataka nini. Vizuri tumalizane vizuri,” alisema.Hata hivyo, Phiri
alisisitiza ataendelea kusubiri apate taarifa ya maandishi na stahiki
zake.
“Kwa mtu aliyeniambia, najua haiwezi kuwa mzaha. Hivyo nitasubiri
barua ili kudhibitisha, pia nitapokea madai yangu, basi nitaaga vizuri
na kurejea nyumbani.”Nafasi ya Phiri inachukuliwa na Goran Kuponovic
raia wa Serbia anayetua leo asubuhi akitokea Hungary.
No comments:
Post a Comment