Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper.
STAA wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper
amewabwatukia baadhi ya watu wanaomsema kuwa kafulia na kudai
hawajitambui na wanapenda kuzungumza vitu....
ambavyo hawana uhakika navyo.
Akizungumza na mwandishi wetu, Wolper alisema anashangazwa na watu
ambao wanaojifanya ni watabiri wa maisha yake wakati hakuna hata mmoja
ambaye anajua ni wapi alipotokea, wanamzushia na kumuandika mitandaoni.
“Jamani kuna watu ambao wanajifanya ni watabiri katika maisha ya watu
na ni vyema kila mtu akafuata mambo yake na kuangalia zaidi vya kwao
na siyo kunifuatilia leo nimefulia au leo niko sawa, wanaboa sana,”
alisema Wolper pasipo kuwataja majina.
No comments:
Post a Comment