NA DK. A. MANDAI
USHAURI SIMU: +255 717 961795
+255 754 391743
LEO katika makala haya tutaeleza dalili za kisukari na wiki ijayo tutafafanua madhara yake. Endelea.
Mgonjwa pia anaweza kuona dalili ya kuchoka haraka, kupungua uzito, vipele mwilini ambavyo kitaalamu huitwa diabetic dermadromes...
Mgonjwa pia anaweza kuona dalili ya kuchoka haraka, kupungua uzito, vipele mwilini ambavyo kitaalamu huitwa diabetic dermadromes...
Wagonjwa wa kisukari pia huwa katika hatari ya kupata maambukizi
katika kibofu cha mkojo, ngozi na kwa wanawake sehemu za siri. Aidha
kuna dalili maalumu ambazo hutokea kwa wagonjwa wa kisukari iwapo
mgonjwa atapatwa na mojawapo ya madhara (complications) ya ugonjwa huo.
Madhara hayo ambayo hujulikana kwa kifupi DKA hutokea kwenye aina ya
kwanza ya kisukari na huwa na dalili zifuatazo: Mgonjwa kutoa harufu ya
acetone inayofanana kidogo na harufu ya pombe.
Mgonjwa pia hupumua kwa haraka na kwa nguvu, kujihisi kichefuchefu, kutapika, kuhisi maumivu ya tumbo na kupoteza fahamu. Kupoteza fahamu mgonjwa kunakoitwa Hyperosmolar Non-ketotic coma hutokea kwenye kisukari cha aina ya pili ambapo mara nyingi husababishwa na upungufu wa maji mwilini.

MATIBABU
Baada ya mtu kuwa na dalili za ugonjwa wa kisukari matibabu huanza baada ya kufanyiwa vipimo na kuthibitisha kwamba kweli ana ugonjwa huo. Baada ya vipimo tunaweza kusema mtu fulani ana kisukari iwapo moja, kiwango cha sukari kwenye damu kitakuwa sawa na 126mg/L, kipimo ambacho kwa kawaida hufanyika kwa mtu ambaye hajala chakula chochote.

Kwa jina lingine kipimo hiki huitwa Fasting Blood Glucose (FBG).
Pili, iwapo kiwango cha sukari kwenye damu kinapokuwa sawa na 200mg/L
kwa mtu ambaye amelishwa gram 75 za glucose ndani ya masaa mawili.
Kipimo hiki pia huitwa Oral Glucose Tolerance Test (OGTT). Au iwapo
mgonjwa atafanyiwa kipimo kinachoitwa glycoslytated hemoglobin (Hb A1C)
na kuwa chanya.
No comments:
Post a Comment