Msanii wa filamu Bongo, Aisha Bui wakati akiwa katika ofisi za kusambaza filamu za Yuneda zilizopo Mbagala.
KESI ya msanii wa filamu Bongo, Aisha Bui ya kufanya
fujo ofisini kwa msambazaji wa filamu akidai kutolipwa fedha zake za
filamu bado ni ya moto ambapo msambazaji anazungumza na mwanasheria wake
kisha kumburuza mwigizaji huyo mahakamani....
Chanzo makini kimedai kuwa, baada ya Aisha kulala polisi na kutoka
kwa dhamana msambazaji huyo, Ngeze Yuneda anatarajia kumburuza
mahakamani akidai amembambikizia madai mengi ya uongo.
Alipoulizwa Aisha kuhusiana na habari hiyo, alisema:
“Hata sielewi kwa sababu walisema wanapeleka faili kwa mwanasheria ndipo tutakapoitwa ili ijulikane inakuwaje, nawasubiri.''
Alipoulizwa Aisha kuhusiana na habari hiyo, alisema:
“Hata sielewi kwa sababu walisema wanapeleka faili kwa mwanasheria ndipo tutakapoitwa ili ijulikane inakuwaje, nawasubiri.''
Aisha Bui akiwa mwenye gadhabu siku ya tukio.
Hivi karibuni Aisha alifanya fujo kwenye ofisi za Yuneda kutokana na
kumuuzia muvi tangu Aprili, mwaka huu lakini hakumpa fedha yoyote na
walikubaliana milioni tisa lakini alikuwa akimpiga kalenda ndipo
akamwangushia timbwili ofisini kwake.
No comments:
Post a Comment