Askofu, Elia Muuno almaarufu kwa jina la Adamu wa Pili, Mungu wa majeshi.
MSHTUKO! Kifo cha Askofu na Nabii wa Kanisa la The Pool of Siloam
lililopo Mbezi-Makonde, Kinondoni, Dar es Salaam, Elia Munuo almaarufu
kwa jina la Adam wa Pili, Mungu wa Majeshi, kimeacha ‘sintofahamu’ kwa
kuwa kiongozi huyo alitabiri na kutangaza tukio hilo na likawa kweli,..
Kwa mujibu wa mashuhuda ambao ni viongozi na baadhi ya waumini wa
kanisa hilo, tukio hilo lilijiri Alhamisi iliyopita ambapo askofu huyo
aliwaita makuhani (Viongozi) kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya
Bongo na kuwaambia mambo manne muhimu.
Mmoja wa waumini wa kanisa la The Pool of Siloam akiwa getini.
Mambo hayo ni pamoja na wosia wake ukiwa na kauli yake ya kusindikiza
safari yake ya mwisho kwa kuwa alikiona kifo chake kuwa kingejiri
mchana wa siku hiyo na kuwataarifu huku akiwa mzima wa afya.
Kwa mujibu wa msemaji wa kanisa hilo, Kuhani, Kiongozi Miaka 1,000 aliwaambia kuwa amekamilisha kujenga msingi wa kanisa la mwisho la kizazi cha nne.
Kwa mujibu wa msemaji wa kanisa hilo, Kuhani, Kiongozi Miaka 1,000 aliwaambia kuwa amekamilisha kujenga msingi wa kanisa la mwisho la kizazi cha nne.
Alifafanua kwamba, baada ya miaka 1,000 ya kanisa, walianza mwaka wa
kwanza ambapo alitambulisha tarehe ya Kimungu (Kirumi) kwa maana hiyo
yeye alifanya kazi ya utumishi kwa miaka 12 na hatimaye aliikamilisha.
“Alifanya kazi kwa muda wa miaka 12 hadi anatwaliwa lakini kwa
kawaida hatuna mwaka wa kumi na ukiangalia miaka yetu tunaanza na 1-9,
halafu tunaanza tena na moja hivyo nabii wetu alikuwa kwenye uongozi kwa
mwaka wa tatu kabla hajatwaliwa na Mungu,” alisema Kuhani.
Lango kuu la kanisa hilo.
Miongoni mwa kile kinachozungumzwa juu ya tukio hilo na kuacha
viulizo kwa makuhani hao ni baada ya kuwaambia kuwa, gari lake lilikuwa
linakuja kumchukua mchana wa siku hiyo bila wao kuelewa alichokuwa
akimaanisha kwa ufasaha.
“Hili liliacha viulizo sana kwa sababu gari lake alimaanisha kuwa ndicho kifo chake na katika miujiza kweli akafa mchana huo.
“Kusema kweli hili kanisa lina bahati sana. Elia tulikuwa naye hapa
japokuwa amekwenda, lakini tumebaki naye kiroho. Tunaamini atarudi kama
Yesu,” alisema kuhani huyo.
No comments:
Post a Comment