Supastaa wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo a.k.a Jide au Jaydee akipozi.
Kutoka moyoni! Wakati kukiwa na maneno mengi juu ya
madai ya kuvunjika kwa ndoa yake na prizenta maarufu Bongo wa Redio
E-FM,...
Gardner G Habash ‘Kepteini’, supastaa wa Bongo Fleva, Judith
Wambura Mbibo a.k.a Jide au Jaydee amefunguka kuwa naye si mkamilifu
kwani siyo Yesu wala Bikira Maria.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, wikiendi iliyopita Jide
aliamua kuvunja ukimya kufuatia maswali ya mashabiki wake lukuki
waliotaka afunguke kinachoendelea katika maisha yake.
Judith Wambura Mbibo a.k.a Jide au Jaydee.
“Watu wanategemea niwe kama Yesu au Bikira Maria? Siwezi, mimi ni
mwanadamu tu. Hakuna aliye mkamilifu. Niacheni niishi maisha yangu bila
stresi. Mwingine yeyote pia aishi maisha yake. Kila mmoja anatakiwa awe
huru,” aliandika Jide.
No comments:
Post a Comment