
Kim Poulsen.
LICHA ya kuwa na msisitizo kuhusiana na suala la Kocha Patrick Phiri kuwa ndiye atabaki kuwa kocha wa Simba, bado juhudi za kumpata Kim Poulsen, ziko palepale.Uongozi wa Simba umeamua kufanya uboreshaji wa kikosi chake na tayari umefanya mazungumzo na Poulsen ambaye yuko kwao Denmark kwa ajili ya kuinoa Simba...
Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza, wajumbe wa
kamati ya utendaji wa klabu hiyo wamegawanyika, wengine wakiamini Phiri
anahitaji muda, lakini wako wanaoamini uwezo wake umeishia hapo na
vizuri nafasi itolewa kwa Poulsen au kocha mwingine.
“Kweli limekuwa ni jambo lenye utata kidogo. Mazungumzo na Poulsen
yako pazuri na inaonekana kama si leo au kesho, lakini atakuja kuinoa
Simba,” kilieleza chanzo.
Kocha wa Simba, Patrick Phiri.
“Phiri ni kocha mwenye heshima Simba. Lakini wako wajumbe wanaona
kidogo kama ameishia hapo, hivyo ni vema kumpa nafasi aende
vizuri.”Poulsen alikuwa akiinoa Taifa Stars baada ya kuchukua nafasi ya
mkongwe Jan Poulsen ambaye pia anatokea Denmark.
Kinachosababisha Simba ianze kujadili suala la kubadili kocha ni
kutokana na kutoka sare sita mfululizo kwenye ligi.Hata hivyo, wapo
ambao wamekuwa wakiamini Phiri hana tatizo, lakini swali limekuwa ni
vipi timu isishinde halafu lawama ziende kwingine?
Uongozi wa Simba umejisafisha katika hilo kwa kuwa umeonyesha kufanya kila kitu kwa wachezaji na timu kwa jumla ili ifanye vema.
No comments:
Post a Comment