Mchezaji wa Azam, Kipre Tchetche.
KUELEKEA dirisha
dogo la usajili, Azam FC imefunguka kuwa ipo tayari kuwauza wachezaji
wake Shomari Kapombe, Kipre Tchetche na Mwadini Ali endapo kutatokea
klabu nyingine inayoweza kutoa dau zuri...
Hatua hiyo inakuja hivi karibuni, baada ya kuripotiwa kuwa Kipre
anaweza kuondoka klabuni hapo kuelekea nchini Malaysia, Sri Lanka au
katika Klabu ya Sofapaka ya nchini Kenya.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Katibu Mkuu wa Azam FC, Idrissa
Nassor, alisema kuwa kama kuna timu itawahitaji wachezaji wao watawauza
lakini kwa dau la uhakika kutokana na viwango vyao.
Nassor alisema kuwa mpaka sasa hakuna mchezaji wa kikosi hicho ambaye
amemaliza mkataba wake ili kuweza kuondoka katika klabu hiyo labda
mpaka pale msimu utakapokuwa unamalizika.
Mchezaji wa Azam Shomari Kapombe.
“Kama kuna timu yoyote ya ndani au nje itawahitaji wachezaji wetu
kama Kipre Tchetche, Shomari Kapombe au Mwadini Ali hatuna tatizo,
kikubwa ni maelewano, ingawa wachezaji hawa wana mkataba,” alisema
Nassor.
No comments:
Post a Comment