Mashabiki wa...
Mbeya City.
WAKATI
ikiendelea kuwa na matokeo mabaya katika Ligi Kuu Bara, uongozi wa Mbeya
City umemkabidhi madaraka kocha wao, Juma Mwambusi kuwaondoa kikosini
wachezaji watakaoonekana hawana umuhimu klabuni hapo wakati wa dirisha
dogo la usajili.
Emmanuel Kimbe ambaye ni katibu wa Mbeya City, ameliambia amefunguka na kusema kuwa, kinachotakiwa ni mwalimu kuwasilisha ripoti kisha kama kuna
wachezaji wa kuondolewa au kuongezwa, wao wataifanyia kazi.
“Tunasubiri mapumziko ya usajili wa dirisha dogo ili kupata ripoti ya
kocha na hapo ndipo tutakapojua nani aondoke na nani aongezwe katika
usajili, lengo letu ni kuona timu inakuwa bora,” alisema Kimbe.Mbeya
City imefungwa michezo mitatu katika ligi kuu na sare mbili, huku ikiwa
imeshinda mchezo mmoja.
No comments:
Post a Comment