Friday, 7 November 2014

PETER MANYIKA APELEKWA ULAYA.

Kipa chipukizi wa Simba,...
Peter Manyika.
KOCHA wa Makipa wa Simba, Zdravko Djokevic, amesema kipa chipukizi wa klabu hiyo, Peter Manyika, ana nafasi kubwa ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi, ikiwemo Ulaya ikiwa atapata maendeleo mazuri.
Zdravko ambaye yupo nchini ikiwa hii ni wiki ya tatu, kwa kazi ya kuwanoa makipa wa Simba, Ivo Mapunda, Hussein Sharif na Manyika, amemsifia kinda huyo kwa kusema kuwa anaweza kuwa msaada mkubwa kwa taifa baadaye kama akitumika vizuri.
Akizungumza na Championi Ijumaa, kocha huyo alisema katika kipindi kifupi alichokaa na Manyika, amegundua kuwa kinda huyo ana uwezo wa kipekee na kipaji chake ni kikubwa.
“Ana uwezo mkubwa, kipaji chake ni cha hali ya juu, kila utakalomuelekeza anaelewa vizuri sana na kulifanyia kazi, nakuhakikishia, miaka ya baadaye atacheza soka nje ya Tanzania hata ikiwezekana Ulaya, niamini,” alisema Zdravko.

No comments:

Post a Comment