Friday, 14 November 2014

NIYONZIMA KUTUA SIMBA!

Kiungo mshambuliaji wa Yanga,..
Haruna Niyonzima.
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima amefunguka kuwa yupo tayari kutua Simba iwapo itamhitaji kwa kuwa mkataba wake na Yanga umebakiza miezi mitano.
Niyonzima ambaye alitua Yanga akitokea APR ya Rwanda, ameliambia gazeti hili kuwa anakaribisha timu yoyote kwa ajili ya mazungumzo ikiwemo Simba kwa kuwa soka ndiyo maisha yake na ndiyo kazi yake.
“Hapa nilipo bado ni mchezaji halali wa Yanga ila nimebakiza kati ya miezi minne na mitano kukamilisha mkataba wangu, ila nipo tayari kusaini timu yoyote ile itakayonihitaji.
“Siyo Simba pekee, yoyote tu ili mradi tukubaliane maslahi,” alisema Niyonzima na kuongeza:  “Kama mambo yasipokuwa mazuri Yanga naweza kurejea nchini kwetu nikacheze huko.”

No comments:

Post a Comment