Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho...
Ngassa na mkewe wakiwa wenye nyuso zenye furaha baada ya kufunga ndoa.BAADA ya kuelezwa kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa ameshindwa kusafiri na Taifa Stars kwenda nchini Afrika Kusini kutokana na matatizo ya kifamilia, imebainika kuwa mchezaji huyo amebaki nchini ili afunge ndoa.
Stars ipo Afrika Kusini kwa ajili ya kambi ya muda kisha ikitarajiwa
kuelekea nchini Swaziland, leo kwa ajili ya mechi ya kirafiki baina ya
mataifa hayo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Somhlolo jijini Mbabane.
Rafiki wa karibu wa Ngassa alizungumza na mwandishi na kusema kuwa, Ngassa
hana matatizo ya kifamilia ila aliomba kubaki nchini kwa kuwa alikuwa
katika hatua za mwisho za kufunga ndoa.
“Ngassa amebaki ili afunge ndoa, shughuli yote itafanyika kesho (leo
Ijumaa) hapahapa Dar, nafikiri hii itakuwa ndoa yake ya tatu,” alisema
rafiki huyo.
Ngassa alipotafutwa kwa njia ya simu ili aweze kuzungumzia ishu iyo lakini simu zake zote zilikuwa
hazipatikani, ndipo akatafutwa baba yake mzazi, Khalfan Ngassa ambaye
alikuwa na haya ya kusema:
“Ndiyo anataka kufunga ndoa, hii itakuwa ndoa yake ya pili siyo ya
tatu, ile ya kwanza ndiyo ya yule mwanamke waliyevurugana na kesi yao
ipo mahakamani, huyo mnayesema wa pili hakufunga naye ndoa bali ni mzazi
mwenziye, huyu wa sasa ndiye atakuwa mke halali.”
No comments:
Post a Comment