.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima
za mwisho kwa mwili wa Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata
Ikulu mjini Lusaka Zambia Novemba 11,2014....
.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal wa kwanza
(kushoto) akiwa na Rais Mstaafu wa Zambia Mhe. Rupia Banda, Rais wa
Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, Rais wa Msumbiji Mhe. Ermando Guebuza na
Kaimu Rais wa Zambia Dkt. Guy Scott kwenye Misa Maalum ya kuaga mwili wa
Rais Michael Sata iliyofanyika Novemba 11,2014 kwenye Uwanja wa Taifa
mjini Lusaka Zambia.
.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na
Katibu Mkuu wa Chama Tawala cha PF Mhe. A.B. Chikwanda kwenye Viwanja
vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa wakati mazishi ya
Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata yaliyofanyika Novemba
11,2014 kwenye uwanja wa Taifa mjini Lusaka Zambia.
.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji Rais
mstaafu wa kwanza Zambia Dkt. Keneth Kaunda mara baada ya kumalizika
maziko ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja
vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika
Novemba 11,2014 mjini Lusaka Zambia.
.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji Rais
mstaafu wa Zambia Mhe. Ruphia Banda baada ya kumalizika mazishi ya Rais
wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja vya Ubalozini
katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika Novemba 11,2014.
katikati Rais mstaafu wa kwanza wa Zambia Dkt. Keneth Kaunda.
.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisaini kitabu
cha maombolezo ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye
Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa
yaliyofanyika Novemba 11,2014.
No comments:
Post a Comment