Dk. RK Gupta aliyetiwa mbaroni...
DAKTARI anayehusishwa na tukio la vifo vya watu 13 katika kituo cha
kutoa huduma ya kuzuia uzazi kwa njia ya upasuaji jimboni Chattisgarh
nchini India, Dk. RK Gupta ametiwa mbaroni.
Baadhi ya akina mama waliofanyiwa upasuaji wakiwa hospitali.
Dk Gupta na msaidizi wake waliwafanyia upasuaji wananawake 83 katika
kijiji cha Pendari ndani ya saa 3 Jumamosi iliyopita na kusababisha vifo
13 huku wengi wakiwa wamelazwa hospitali, 20 kati yao wakiwa katika
hali mbaya.
Rais wa India, Ram Avtar aliyempoteza mke wake aitwaye, Nem Bai akiomboleza na wanaye huko Bilaspur, Chattisgarh.
Serikali nchini humo inamtaka daktari mmoja kutoa huduma ya upasuaji kwa watu 35 tu kwa siku.
Ndugu na jamaa wakiomboleza kifo cha mama mmoja aliyefariki baada ya upasuaji huo.
Maandamano yamefanyika baada ya tukio hilo la vifo, huku serikali ya
Jimbo la Chhattisgarh ikitoa amri ya kufanyika kwa uchunguzi.
No comments:
Post a Comment