Mchezaji wa Simba, Amri Kiemba.
BAADA
ya mchakato wa kuchanganua mambo, kuna asilimia kubwa Kamati ya
Utendaji ya Simba ikatoa majibu ya kuwaondoa wachezaji wawili, Amri
Kiemba na Haruna Chanongo.Lakini kiungo mkongwe, Shabani Kisiga anapewa
nafasi ya kuendelea kuitumikia timu hiyo kutokana na utetezi wake..
Watatu hao walisimamishwa kwa tuhuma za utovu wa nidhamu na kucheza
chini ya kiwango na baadaye wakaonyesha utovu wa nidhamu kwa kushindwa
kutokea kwenye kikao cha viongozi.“Wachezaji walivyojieleza, inaonekana
Kisiga amekuwa hana matatizo makubwa na hata imefikia kwamba
atasamehewa.
Mchezaji wa Simba, Haruna Chanongo.
“Lakini Kiemba na Chanongo, kuna zaidi ya asilimia tisini wataondoka
Simba. Sijui, labda mambo yabadilike tena mwishoni, si unajua uongozi ni
kitu cha watu wengi,” kilieleza chanzo.“Watu wengi hawajui uongozi
unafanya nini, ukweli ni kwamba uongozi unajua kila kitu, unajua mambo
mengi kuliko watu wanavyojua na wala hauna nia ya kumuonea mtu, lengo
kuisaidia timu.”
Uongozi wa Simba, bado haujatangaza lolote kuhusiana na hilo lakini
utakuwa na nafasi ya kumalizia uamuzi huo na kuutangaza ndani ya wiki
hii.
Mara baada ya mchezo wa jana ambao Simba walipata ushindi wa bao 1-0
dhidi Ruvu Shooting, Kisiga pekee ndiye alishuka chini baada ya mchezo
kumalizika na kwenda kuwapongeza wachezaji wenzake vyumbani.Hata hivyo,
kocha wa Simba, Patrick Phiri, alipoulizwa kama suala lake limekwisha,
alisema waulizwe viongozi.
No comments:
Post a Comment