Mshambuliaji waSimba,raia wa Uganda Emmanuel Okwi.
BAADA ya
matokeo ya sare sita mfululizo, hatimaye Simba imepata ushindi wake wa
kwanza katika mechi ya saba kwa kuifunga Ruvu Shooting bao 1-0 katika
Ligi Kuu Bara, jana, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam...
Ushindi huo uliwazima kabisa mashabiki wa kundi maarufu la wanachama
waliosimamishwa uanachama la Simba Ukawa ambao wamekuwa wakidai Simba
itatoa sare saba mfululizo na mambo yatakuwa mabaya zaidi kama
wasiporudishwa, wengi wakiamini wana nguvu ya ushirikina.
Alikuwa ni mshambuliaji raia wa Uganda, Emmanuel Okwi, aliyefuta
mzimu wa sare kwa kufunga bao zuri katika dakika ya 76 baada ya kufanya
kazi nzuri yeye mwenyewe pamoja na Elius Maguli.Okwi aliumiliki mpira
mbele ya mabeki wa Ruvu na kutoa pasi kwa Maguli ambaye alipiga shuti
kali lililopanguliwa na kipa wa Ruvu, Abdallah Rashid kisha Okwi
akamalizia kazi kwa kuutupia mpira wavuni.
Ushindi huo umeifanya Simba kufikisha pointi tisa na kuwa ushindi
wake wa kwanza katika ligi kuu ya msimu huu.Simba ilionyesha kuwa na nia
ya kupata ushindi katika mechi hiyo lakini upinzani ulikuwa mkali. Ruvu
walionekana kuwa wagumu kufungika licha ya Simba kupata kona tisa huku
wao wakiwa hawana hata moja kwenye mchezo huo.
Staika wa Simba, Amissi Tambwe alishindwa kuitumia nafasi ya kufunga
katika dakika ya 37 baada ya kuwapita vizuri mabeki wa Ruvu kisha kupiga
shuti lililotua mikononi mwa Abdallah.Kocha wa Simba, Patrick Phiri
ambaye alionekana kuwa na furaha kubwa mara baada ya mchezo huo, alisema
kikosi chake kinaimarika siku baada ya siku.
Kocha wa Ruvu, Tom Olaba alisema: “Timu yangu imecheza vizuri lakini
kutotumia nafasi vizuri tulizopata ndiyo kumesababisha tufungwe.” Lakini
msemaji wa Ruvu, Masau Bwire, ambaye amekuwa na maneno mengi, alipata
kashkashi kutoka kwa mashabiki waliokuwa wakimzonga baada ya mchezo na
baadaye akasema walifurahi kumuona na walitaka kupiga naye picha tu.
Wakati huohuo, Okwi amefichua siri kuwa alimlazimisha kocha wake,
Patrick Phiri ampange licha ya kujua kuwa alikuwa akisumbuliwa na
maumivu ya mguu.“Nilikuwa nasumbuliwa na mguu muda mrefu tu, kocha
anajua na hata daktari wa timu anajua hilo, walitaka nipumzishwe lakini
sikukubali kwa kuwa niliona wachezaji wengi ni chipukizi, bila sisi
wazoefu kukomaa hali ingezidi kuwa mbaya.
“Naipenda sana Simba ndiyo maana nililazimika kumwambia kocha anipange hivyohivyo tu,” alisema Okwi mara baada ya mechi ya jana.
Simba Ukawa wawekewa ulinzi mkali Taifa
Mashabiki wa kundi la Simba Ukawa walilazimika kuingia wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari.
Mashabiki hao ambao huwa na kawaida ya kushangilia mwanzo mwisho kila Simba inapocheza, waliingilia upande unaoaminika kuwa ni wa Simba kisha wakati wa kutoka wakatokea upande unaoaminika kuwa ni wa Yanga wakiwa chini ya ulinzi mkali.
Simba Ukawa wawekewa ulinzi mkali Taifa
Mashabiki wa kundi la Simba Ukawa walilazimika kuingia wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari.
Mashabiki hao ambao huwa na kawaida ya kushangilia mwanzo mwisho kila Simba inapocheza, waliingilia upande unaoaminika kuwa ni wa Simba kisha wakati wa kutoka wakatokea upande unaoaminika kuwa ni wa Yanga wakiwa chini ya ulinzi mkali.
Mara baada ya kufika eneo la kuegesha magari, mashabiki hao walikaa
kwa muda wakisubiri gari lao wakiwa chini ya askari 11 na walinzi
wengine nane wa uwanjani hapo, muda mfupi baadaye gari aina ya Coaster
lenye namba T746 DBW lilifika na kuwachukua kuondoka uwanjani hapo huku
likilindwa na magari matatu yaliyokuwa na sakari.
Wakati kikundi hicho kikiondoka uwanjani hapo, kulikuwa na majibizano
ya chini kwa chini kati yao na mashabiki wengine wa Simba ambao baadhi
walikuwa kwenye maeneo tofauti ndani hadi nje ya uwanja wakiwasubiri
watoke, lakini walitoka salama.
No comments:
Post a Comment