Friday, 31 October 2014

UFUPI WAMSUMBUA STEVE NYERERE KWA AUNT EZEKIEL


Ufupi alionao aliyekuwa Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ unaonekana kumtesa na hivi karibuni alikutana na mazingira magumu alipokuwa akitaka kumhagi msanii mwenzake Aunty Ezekiel........

 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ akihaha kumhagi Aunty Ezekiel.
Tukio hilo lilijiri kwenye pati ya bethidei ya Aunty iliyofanyika kwenye hoteli moja iliyopo Masaki jijini Dar ambapo wakati wa keki, Steve alilishwa kwa Aunty kuinama kidogo lakini wakati wa kukumbatiana, jamaa huyo aliishia kwenye kifua na alipojaribu kujirefusha ili ambusu, alishindwa hivyo kuibua kicheko ukumbini hapo.
 
‘Steve Nyerere’ akijiinua kujaribu kumfikia aunty ezekiel.
Hata hivyo, kuonesha kumuonea huruma, Aunty aliyekuwa amevalia viatu virefu aliinama kidogo na kufanikisha zaezi hilo ambapo mmoja wa wahudhuriaji alisikika akisema; ‘Steve umezidi ufupi na wewe’.

No comments:

Post a Comment