Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu.
BAADA ya serikali
kutoa siku saba za uchunguzi wa sakata la umri wa Miss Tanzania 2014,
Sitti Mtemvu, maamuzi ya uchunguzi huo yameendelea kuwa katika hali ya
sintofahamu baada ya kila upande kuonekana kutokuwa tayari kuweka wazi
juu ya kinachoendelea.
Wiki iliyopita, Naibu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Juma Nkamia, alisema kuwa wametoa siku saba kwa Baraza la Sanaa
Tanzania (Basata) kufanya uchunguzi juu ya suala hilo lakini mpaka jana
hakuna ripoti iliyokuwa imetolewa.
Championi Ijumaa lilizungumza na Ofisa Habari wa Basata, Aristides
Kwizela ambapo alisema uchunguzi wa suala hilo bado haujakamilika.“Ni
kweli siku saba zimepita lakini bado uchunguzi haujakamilika, hatuwezi
kusema utakamilika lini ila ufafanuzi utatolewa tu,” alisema Kwizela.
Alipotafutwa Waziri Nkamia alisema kwa kifupi: “Nipo jimboni, bado
sijajua kuhusu majibu ya uchunguzi huo, nafikiri ungewauliza Basata
wanaweza kuwa na jibu sahihi.”Kumekuwa na madai kuwa Sitti alidanganya
umri wake kuwa siyo miaka 23 bali ni 25, kitu ambacho ni kinyume na
kanuni za shindano la Miss Tanzania ambapo mwisho wa umri kwa washiriki
ni miaka 24.
No comments:
Post a Comment