Straika wa Simba, Amissi....
Tambwe
KUTOKANA
na kuibuka kwa taarifa kuwa kiwango chake kimeshuka na yupo mbioni
kuondoka Simba, straika wa timu hiyo, Amissi Tambwe, ameamua kufunguka
na kuweka wazi sababu zitakazomuondoa klabuni hapo.
Tambwe ameliambia gazeti hili kuwa, yupo tayari kuondoka Simba licha
ya kuwa bado anaipenda klabu hiyo lakini sababu kubwa ni maneno
anayosingiziwa na manyanyaso anayopata klabuni hapo.
“Kabla ligi haijaanza, nilipatwa na hofu baada ya kuambiwa kuwa
uongozi unataka kuachana na mimi ili nafasi yangu ichukuliwe na
(Emmanuel) Okwi, hali hiyo ilinifanya nipoteze mudi ya mazoezi kutokana
na kutumia muda mwingi kufikiria hali hiyo.
“Baada ya siku chache, viongozi hao waliibua jambo jingine tena, hilo
lilikuwa ni lile la kuniondoa katika orodha ya wachezaji watakaosafiri
kwa ndege kwenda Mtwara katika mechi dhidi ya Ndanda FC, si unakumbuka?
“Nilisafiri kwa basi kwenda na kurudi huku wenzangu wakipanda ndege, hakika niliumia sana.
“Lakini kitendo cha hivi karibuni cha kunisingizia kuwa ninaihujumu timu pia kinanifanya niwe na wakati mgumu na kujikuta nikitumia muda mwingi kufikiria mambo hayo, ndiyo maana kiwango changu kimeshuka ukilinganisha na msimu uliopita ambao nilikuwa na amani,” alisema Tambwe ambaye ni mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita.
“Lakini kitendo cha hivi karibuni cha kunisingizia kuwa ninaihujumu timu pia kinanifanya niwe na wakati mgumu na kujikuta nikitumia muda mwingi kufikiria mambo hayo, ndiyo maana kiwango changu kimeshuka ukilinganisha na msimu uliopita ambao nilikuwa na amani,” alisema Tambwe ambaye ni mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita.
Kuhusiana na mpango wa kujiunga na Yanga, Tambwe alisema: “Habari
hizo za kujiunga na Yanga hazina ukweli wowote na zinalenga kutaka
kunichonganisha na viongozi wangu, mimi ni mali ya Simba.
“Ndiyo, Yanga waliwahi kunihitaji lakini hiyo ni zamani, siyo sasa,
walinifuata msimu uliopita nikawaambia wafuate taratibu zinazotakiwa kwa
kuwa nilikuwa bado nina mkataba mrefu na Simba. Kama bado wana nia na
mimi wafuate tu mchakato unaotakiwa.”
Akizungumzia juu ya Tambwe kuondoka klabuni hapo, Ofisa Habari wa
Simba, Humphrey Nyasio, mapema wiki hii alinukuliwa akisema:“Tambwe bado
ni mchezaji wetu na ataendelea kuwa klabuni hapa kwa kipindi chote cha
mkataba wake na bado tunamhitaji.”
No comments:
Post a Comment