Kocha wa Simba, Patrick.....
Phiri.
SIKU mbili baada ya kauli ya uongozi wa Simba kuwa
umetoa mechi mbili kwa benchi la ufundi kuhakikisha linashinda mechi
hizo zote, la sivyo timuatimua itawadia, Kocha wa Simba, Patrick Phiri,
amezungumzia juu ya masharti hayo na kuyagomea kimtindo.
Simba imepata matokeo ya sare tano mfululizo katika Ligi Kuu Bara,
ndipo Phiri akaliambia gazeti hili kuwa, masharti hayo siyo muhimu kwake
kwa kuwa anachotaka siku zote ni ushindi, hivyo suala la kupewa mechi
mbili halina nafasi kwake kwa kuwa yeye anapigana ashinde mechi zote na
wala siyo mechi mbili alizopewa.
“Sikuja Tanzania kupata ushindi wa mechi mbili pekee, nimesikia
kuhusu agizo la mechi mbili lakini kwangu siliweki jambo hilo kichwani.
Muhimu zaidi kwangu ni kushinda kila mechi iliyo mbele yangu.“Nafahamu
kwamba timu ipo kwenye kipindi kigumu katika kutafuta ushindi, hata mimi
pia nimekuwa sijisikii amani katika suala hili.
“Nimekuja Tanzania kwa ajili ya Simba ishinde lakini bado sijafanikiwa,” alisema Phiri na kuongeza:
“Wala sitakuwa na presha ya kuondolewa kwenye timu, kama kutakuwa na hayo mengine tutajua hapo baadaye.”
“Wala sitakuwa na presha ya kuondolewa kwenye timu, kama kutakuwa na hayo mengine tutajua hapo baadaye.”
Wakati hayo yakiendelea, mwenyekiti wa zamani wa Simba, Ismail Aden
Rage, ameibuka na kuupinga vikali uongozi wa klabu hiyo kwa kitendo cha
kutaka kumfukuza Phiri.
“Hakuna sababu yoyote inayoweza kusababisha uongozi kumfukuza Phiri
kwa kipindi hiki, naamini kwa kufanya hivyo timu itazidi kufanya vibaya
kwa sababu mbinu zake wachezaji wameshazizoea.
“Naushauri uongozi wa (Evans) Aveva (rais wa Simba), umpe muda kwa
kuwa timu ipo kwenye mpito,” alisema Rage na kuongeza:“Unajua Simba
walikosea kumtosa yule Mkenya (Donald) Musoti, ni afadhali wangempunguza
(Pierre) Kwizera.”
No comments:
Post a Comment