Wednesday, 29 October 2014

ROKETI YALIPUKA NCHINI MAREKANI


Roketi Antares ikilipuka.

Taswira baada ya mlipuko huo.
Roketi hiyo wakati ikjiandaa kupaa.
ROKETI ya safari za anga za juu iliyokuwa ikielekea Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu imelipuka wakati ikiruka kutoka Jimbo la Virginia nchini Marekani.
Roketi hiyo iitwayo Antares, yenye urefu wa ghorofa 14 ikiwa iliyotengenezwa na Shirika la Orbital Sciences Corp, ililipuka sekunde chache baada ya kuruka katika kituo cha Wallops Flight Facility.
Chanzo cha kulipuka kwa roketi hiyo ya mizigo bado hakijafahamika.
Antares ilitarajiwa kuwa roketi ya tatu kupewa kandarasi na shirika la taifa la kusimamia safari za anga za juu la Marekani, NASA.
Roketi hiyo ilitarajiwa kubeba takribani kilo 2,200 za shehena kwa ajili ya wanaanga sita walioko katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.
"Tutajua kilichotokea hivi karibuni na tutaendelea vizuri na mipango yetu," amesema Frank Culbertson, Makamu wa Rais Mtendaji wa Shirika la Orbital Sciences.
"Wote tumeona hili jambo likitokea kabla katika shughuli zetu na tumeona kampuni husika zikiimarika kutokana na tukio kama hili, na tutafanya vivyo hivyo" aliongeza Frank.

No comments:

Post a Comment