Wafanyakazi kampuni inayomiliki lori hilo ambayo bado haijafahamika, wakifanya tathmini ya hasara iliyopatikana.
Madereva wa bodaboda wakiwa wameacha shughuli zao ili kushuhudia tukio hilo.
LORI
la mafuta aina ya Scania likiwa limesheheni dizeli likitokea bandarini
jijini Dar es Salaam kuelekea mikoani, liligonga tuta katika Barabara ya
Morogoro, eneo la Kimara-Baruti, likapoteza mwelekeo na kupinduka
kisha kuwaka moto na kuteketea kabisa.
Wakati lori
hilo likiwaka, mafuta yenye moto yalisambaa na kutaka kuunguza nyumba za
jirani lakini Kikosi cha Uokoaji na Zima Moto cha Halmashauri ya Jiji,
kiliwahi kufika eneo la tukio na kuudhibiti moto huo.
Tukio hilo limesababisha usumbufu mkubwa kwa magari yanayotumia njia hiyo kutokana na sehemu hiyo kupitika kwa shida.
Tukio hilo limesababisha usumbufu mkubwa kwa magari yanayotumia njia hiyo kutokana na sehemu hiyo kupitika kwa shida.
No comments:
Post a Comment