

Kcha mkuu wa Simba Mzambia, Patrick Phiri
UONGOZI wa Klabu ya Simba chini ya kamati ya
utendaji, umelipa benchi la ufundi la kikosi chao mechi mbili za
kubadili mwenendo wa matokeo ya timu na kuhakikisha timu inapata ushindi
na kucheza mpira unaovutia.
Tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara msimu huu, Simba imekuwa ikipata
matokeo yasiyovutia huku ikicheza michezo mitano na kuambulia pointi
tano jambo lililoilazimu kamati ya utendaji kukaa na kujadili mwenendo
wa timu.
Akizungumza na Championi Jumatano, Katibu Mkuu wa Simba, Stephen
Ally, alisema uongozi wa klabu hiyo, ulikaa kikao juzi Jumatatu katika
Hoteli ya JB Belmont jijini Dar na kuazimia kuwa benchi la ufundi
linaloongozwa na Kocha Mzambia, Patrick Phiri, lipewe mechi mbili na
baada ya mechi hizo kamati itakaa na kujadili matokeo yatakayokuwa
yamepatikana na pia kuchukua uamuzi juu ya benchi hilo.
Stephen aliongeza kuwa uongozi, umewatekelezea yote walioomba kama
benchi ili kuhakikisha timu inafanya vyema katika msimu huu ila kwa
mechi tano za awali, bado timu haijaibuka na matokeo yenye kuridhisha.
“Kabla ya msimu kuanza, timu iliweka kambi Zanzibar na ikaendelea
kukaa kwa wiki mbili baada ya ligi kuanza na baadaye kuweka tena kambi
hapa Dar. Kuna kipindi timu ilienda kambi nchini Afrika Kusini lakini
bado haifanyi vizuri, hivyo benchi la ufundi limepewa mechi mbili
kubadili mwenendo wa matokeo ya timu,” alisema Ally.
.
No comments:
Post a Comment