

Gari aina ya Toyota Hiace likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali hiyo iliyotokea eneo la makumira wilayani Arumeru jana.
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo.
Lori la mafuta lenye namba za usajili T582 ACR baada ya ajali hiyo.
WATU 12 wamefariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea katika
eneo la Makumira wilayani Arumeru baada ya basi dogo aina ya Hiace
kugongana uso kwa uso na lori la mafuta.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Arusha, Lebaratus Sabas amesema ajali
hiyo ilitokea jana majira ya saa 10 jioni baada ya basi hilo dogo aina
ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T519 DBV lililokuwa likitokea
jijini Arusha kwenda Usa River kuhama kwenye saiti yake na kukutana uso
kwa uso na lori hilo la mafuta lenye namba za usajili T582 ACR lilikuwa
linatoka Moshi kwenda Arusha.
Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni
uzembe wa dereva wa basi dogo na wameziomba mamlaka zinazohusika
kuongeza adhabu kwa madereva wazembe.
No comments:
Post a Comment