
Daladala aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T383 CHC ikiwa eneo la Kinondoni.

Raia wakishuhudia ugomvi uliokuwa ukiendelea baina ya madereva wa daladala hizo.
Magari mawili ya daladala aina ya Toyota
Coaster, yanayofanya safari zake kati ya Makumbusho na Kariakoo,
yamepigana pasi (kukwanguana pembeni) eneo la Kinondoni Kanisani jijini
Dar wakati yakigombea abiria na kusababisha tafrani ya aina yake.
Tukio hilo lilitokea mishale ya mchana
baada ya daladala moja ambalo namba zake za usajili hazikufahamika mara
moja, kuvunja 'sight mirror' ya gari lingine lenye namba za usajili,
T383 CHC baada ya dereva wa gari hilo, kumzuia asimpite. Baada ya tukio
hilo, gari lililosababisha ajali lilijaribu kukimbia, yakaanza
kufukuzana mpaka Kinondoni Manyanya ambapo aliyevunjiwa 'sight mirror'
alimpita mwenzake na kupaki mbele yake, songombingo kubwa ikafuatia.
No comments:
Post a Comment