
Mtoto mmoja aliyejulikana kwa jina la Paulina (14) mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Boko, jijini Dar amekatisha masomo kutokana na kupata ujauzito....
Mtoto anayejulikana kwa jina la Paulina (14) alitundikwa mimba na mawanafunzi mwenzake.
Akizungumza kwa huzuni huku akilia, mtoto huyo alisema kwa sasa
haendi shuleni kutokana na kuwa na ujauzito wa miezi miwili alioupata
kwa kijana aliyemtaja kwa jina moja la Paulo mkazi wa Mbweni ambaye ni
mwanafunzi wa sekondari. Alisema.........
“Paulo alikuwa rafiki wa kaka yangu na
alikuwa akija sana nyumbani kwetu, tukawa tumezoeana sana na siku moja
akanishawishi twende kwao, tukaenda na huko ndiyo tukafanya mapenzi
baada ya kuniambia atanioa nikimaliza shule.
Mama mzazi wa Paulina, Luciana John ‘Mama Paulina’ (kushoto) akiwa na mwanaye huyo.
“Alikuwa akinipa fedha mara nyingine elfu mbili au tatu ambazo
nilikuwa nikizitumia shuleni, mwishowe ndiyo nikanasa,” alisema Paulina.
Akizungumza kwa huzuni mama wa mtoto huyo ambaye kazi yake ni kugonga
mawe maeneo ya Chasimba, Boko, Luciana John ‘Mama Paulina’ alisema
anaumia sana kwani alikuwa akitegemea mwanaye asome ili aje kumtoa
kwenye shida lakini badala yake amepata mimba tena ya utotoni.
Imeelezwa kuwa, tukio hilo limefikishwa kwenye vyombo vya sheria ili binti huyo aweze kusaidiwa.
Imeelezwa kuwa, tukio hilo limefikishwa kwenye vyombo vya sheria ili binti huyo aweze kusaidiwa.
No comments:
Post a Comment