
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rashidi Makwiro ‘Chid Benz’ alijikuta akizodolewa na mahabusu wenzake mara baada ya kuingizwa katika Karandinga kupelekwa Segerea baada ya kukosa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu....
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rashidi Makwiro ‘Chid Benz’ akiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 28, mwaka huu ambapo Chid Benz alikuwa
akipelekwa Segerea huku mahabusu waliokuwemo ndani ya gari hilo wakitoa
maneno ya kumkejeli pale alipokosa kiti na kulazimika kusimana.
Mmoja wa mahabusu alisikika akimzodoa
Chid Benz kwa kumwambia: ‘Ustaa wako hukohuko, simama’ ambapo msanii
huyo hakuleta ubishi, alisimama na safari ya kuelekea Segerea ikaanza.
Chid Benz akiwa chini ya ulinzi mkali Mahakamani hapo.
Chid Benz anadaiwa kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya Heroine
yenye thamani ya Tsh. 38,638, Bangi zenye thamani ya Tsh. 1,720 pamoja
na vifaa vya utumiaji wa kuvuta dawa hizo ambapo alikana mashitaka hayo
na kurudishwa rumande hadi Novemba 11, mwaka huu kesi yake itakapotajwa
tena.
No comments:
Post a Comment