Mkurugezi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa, John Nkoma
akizungumza na Bloggers (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa leo....
Baadhi ya wamiliki wa Blogs nchini wakifuatilia mkutano huo.
Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Injinia Andrew Kisaka akitoa mada katika mkutano na Bloggers leo.
Profesa
Nkoma (kushoto) pamoja na Ofisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo, Aron
Msigwa (kulia) wakisikiliza maswali kutoka kwa wamiliki wa Blogs
(hawapo pichani).
WAMILIKI wa Blogs nchini wametakiwa kuzitumia vyema blog zao katika
kuripoti habari na matukio mbalimbali wakati wa uchaguzi wa serikali za
mitaa, wabunge na urais.
Hayo yamesemwa na Mkurugezi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA), Profesa John Nkoma leo alipokuwa akizungumza na wamiliki wa
Blogs hizo katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Profesa Nkoma alisisitiza kwamba wakati wa uchaguzi wamiliki wa Blogs
wanatakiwa kutoa fursa sawa kwa kila upande pasipo upendeleo wowote.
Aidha katika mkutao huo, wamiliki wa Blogs walikubaliana kuendeleza
mchakato wa kuwa na umoja wao uliosajiliwa kisheria ambapo walichagua
viongozi wa muda watakaosimamia mchakato huo.
Uongozi wa muda uliopitishwa na wamiliki hao ni kama ifuatavyo:
1.Joachim Mushi - Mwenyekiti
2. Francis Godwin - Makamu Mwenyekiti
3. Khadija Kalili - Katibu
4. Shamim Mwasha - Mjumbe
5. Othman Maulid - Mjumbe
6. William Malecela 'Lemutuz'- Mjumbe
7.Henry Mdimu - Mjumbe
No comments:
Post a Comment