Rais Michael Sata enzi za uhai wake.
Mazishi ya kitaifa yanafanyika nchini Zambia kumuaga hayati Rais wa
nchi hiyo Michael Sata aliyefariki hospitalini mjini London Uingereza
mwezi jana.Sata alikuwa na umri wa miaka 77...
Katika wiki chache zilizopita, wanachi wamekuwa wakitoa heshima zao
za mwisho kwa kiongozi huyo ambaye mwili wake ulikuwa umelazwa katika
majengo ya bunge.

Mwili wa Rais Michael Satta ukipewa heshima za mwisho.
Rais Sata alifariki akipokea matibabu mjini London UingerezaMazishi
yanayofanyika mjini Lusaka yatahudhuriwa na viongozi mbali mbali wa
kikanda.Rais Sata atazikwa katika eneo lenye makaburi yaliyotengewa
Marais wa nchi hiyo.Taifa hilo kwa sasa linaongozwa na kaimu Rais huku
uchaguzi mkuu ukipangwa kufanyika katika muda wa miezi michache ijayo.
No comments:
Post a Comment