Mtangazaji Penniel Mungilwa 'Penniel'...
MTANGAZAJI
aliyewahi kujiachia kimalovee na Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel
Mungilwa ‘Penny’ amesema mwanamuziki huyo kwa sasa alie tu kwani
ameshachumbiwa na hawezi kumpata tena.
Kauli ya mwanadada huyo ilikuja baada ya kuulizwa kama anaafikiana na
kauli ya mama wa Wema Sepetu, Miriam Sepetu kwamba, kwa kuwa Wema
kamuacha Diomond basi staa huyo wa Wimbo wa Mdogomdogo bora akampose
yeye.
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
“Mmh! Hapa suala la Diamond kurudiana na mimi halipo kabisa maana
simhitaji yeye wala mwanaume mwingine yeyote, mimi ninaye wangu tayari
ambaye ameshanichumbia hivyo sitarajii kabisa kuwa na mwingine zaidi
yake,” alisema Penny.
No comments:
Post a Comment